Orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Ajira Portal 2025/2026 walioajiriwa kada mbalimbali Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 02 Septemba 2024 na 12 Januari 2025, 20-01-2024 na tarehe 17-01-2025 kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Maelekezo kwa Waombaji Waliofaulu
Waombaji waliofaulu usaili wanapaswa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili.
Baada ya muda huo kuisha, barua ambazo hazitachukuliwa zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao za Posta.
Waombaji kazi waliofaulu na kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliobainishwa kwenye barua zao, wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua za ajira.
Waombaji ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili wanatambuliwa kuwa hawakufaulu usaili, hivyo wanashauriwa kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa.
Walioajiriwa February, 2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI (05-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA (04-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA (04-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI (04-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI (03-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI (03-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI (02-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA ZA WALIMU (01-02-2025)
MUHIMU:
Wanaofika kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi lazima wawe na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Leseni ya Udereva
Hongereni kwa waliofanikiwa!
Kwa wale ambao hawajafaulu, msiache kujaribu tena nafasi zitakapotangazwa!