Kuitwa kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026

Orodha ya majina ya walioitwa Kuitwa kwenye Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025/2026 immigration. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kuripoti katika Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga, kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga – Mkoani Tanga, siku ya Jumamosi, tarehe 01 Machi 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana. Mwanafunzi atakayekosa kuripoti ndani ya muda uliotajwa hatapokelewa.

Nafasi za Kazi Ajira Portal

Kwa waliochaguliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kuripoti katika Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (Tunguu) siku ya Jumatatu, tarehe 24 Februari 2025, saa 2:00 asubuhi.

Walioitwa kwenye Mafunzo Uhamiaji

1. Nyaraka Muhimu kwa Mwanafunzi

Mwanafunzi anatakiwa kuripoti akiwa na vyeti halisi vya elimu na fani mbalimbali. Asiyekuwa na nyaraka halisi hatapokelewa chuoni.
Nyaraka zinazohitajika ni:

  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba
  • Vyeti halisi vya elimu: Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na Shahada
  • Vyeti vya ujuzi mbalimbali (kwa wenye ujuzi)

2. Vifaa na Mahitaji Muhimu

Mwanafunzi anatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo:

  • Fedha Tsh. 50,400/= kwa Bima ya Afya (kwa wasio na bima au wenye bima inayokwisha kabla ya tarehe 31/12/2025)
  • Fedha Tsh. 25,000/= kwa ajili ya vipimo vya afya
  • Fedha za kujikimu kwa matumizi binafsi
  • Truck suit (02) – rangi nyeusi na dark blue
  • Raba za michezo jozi (02) – rangi yoyote
  • Nguo nadhifu za kiraia jozi (03)
  • Mashuka (04) – rangi ya bluu
  • Mto wa kulalia (01) na foronya (02) – rangi ya bluu
  • Chandarua (01) – rangi ya bluu
  • Madaftari makubwa (04) – 4QRs
  • Sanduku la chuma (Trunker)
  • Ndoo za plastiki (02) – moja ya lita 10 na moja ya lita 20
  • Fulana (02) – rangi ya dark blue zenye shingo ya duara
  • Viatu vya mvua (rain boots) jozi (01)
  • Taulo (01)
  • Kandambili jozi (01)
  • Vifaa vya usafi:
    • Jembe (01) na mpini wake
    • Fyekeo (01)
    • Panga (01)
    • Rake (01)

Tafadhali fahamu: Vifaa hivi vinapatikana katika Duka la Chuo, hivyo mwanafunzi anaweza kuvinunua kwa ridhaa yake.

3. Angalizo Muhimu

  • Gharama za usafiri kutoka nyumbani hadi chuoni zitabebwa na mwanafunzi mwenyewe.
  • Wanafunzi watafanyiwa uchunguzi wa afya kabla ya kuanza mafunzo. Wale watakaobainika kuwa na changamoto za kiafya hawataruhusiwa kujiunga na Chuo.

Orodha ya majina ya waliochaguliwa inapatikana kwenye tovuti ya Idara ya Uhamiaji: www.immigration.go.tz

Download PDF

Jukwaa Forum
Logo
Shopping cart