Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe kwa kushirikiana na shirika la USAID Afya Yangu (My Health) Southern Project imekuwa ikitekeleza Afua za kupambana na VVU/UKIMWI na Kifua kikuu katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inakaribisha maombi ya kazi ya muda (Miezi kumi) kutoka kwa Watanzania wenye sifa, uwezo na ujuzi wa taaluma za Afya. Watumishi watapangiwa kufanya kazi katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya vilivyopo katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:
WAPIMAJI VVU WA HIYARI – NAFASI 30
(Njombe Mji 7, Mji wa Makambako 1, Njombe Vijijini 8, Makete 3, Ludewa 5, Wanging’ombe 6)
Majukumu ya kazi
i. Uhamasishaji na elimu juu ya uwepo wa Huduma za Kupima VVU (HTS) yaani kuwaelimisha wateja juu ya masuala yote ya magonjwa ya VVU na usimamizi wa matibabu pamoja na maisha ya kimsingi ya afya.
ii. Kuhakikisha upimaji wa VVU kwa washirika wa ngono wa wateja wanaopokea huduma unafanyika kwa usahihi na kuwajulisha.
iii. Kushirikiana na watoa huduma wa Afya wa kituo husika na kuhakikisha usimamizi wa huduma bora za upimaji wa VVU kwa wateja.
Malengo Tarajiwa
i. Kuhakikisha upimaji wa VVU kwa washirika wa ngono wa wateja wanaopokea huduma (Index Testing) unakubalika kwa zaidi ya asilimia 98 kwa wateja wapya (TX-NEW), wapokea huduma wenye idadi kubwa ya wingi wa VVU na wapokea huduma waliyorudi kwenye tiba baada ya kupotea (TX_RTT) kwa mwezi husika.
ii. Kuhakikisha anawatambua na kuwafikia washirika sahihi wa ngono wa wapokea huduma angalau wawili kwa kila mmoja.
iii. Kuhakikisha upimaji wa zaidi ya asilimia 98 kwa washirika wa ngono wa wapokea huduma waliotambulika.
iv. Kuhakikisha anawatambua na kuwafikia angalau watoto watatu wa kibaolojia wa wapokea huduma.
v. Kuhakikisha upimaji wa zaidi ya asilimia 98 kwa watoto wa kibaolojia wa wapokea huduma waliotambulika.
vi. Kufikisha malengo ya siku na mwezi za upimaji VVU ikiwamo upimaji wa VVU kwa washirika wa ngono wa wapokea huduma, upimaji wa VVU unaoanzishwa na mtumishi wa afya, upimaji binafsi wa VVU, upimaji wa washirika wenye tabia sawa hatarishi kwa maambukizi ya VVU na dawa kinga kuzuia kupata maambukizi ya VVU (PrEP).
Sifa za mwombaji
i. Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) na waliohitimu mafunzo ya Astashahada/Stashahada katika Fani ya Uuguzi/utabibu/maabara.
ii. Awe na leseni hai ya Kutoa Huduma (valid practice license), muombaji mwenye mafunzo na cheti cha upimaji VVU atapewa kipaumbele.
iii. Awe mwenye uzoefu wa kufanya kazi walau miezi sita katika vituo vya Tiba na Matunzo vilivyopo Mkoani Njombe.
iv. Awe na ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
v. Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
vi. Awe muadilifu na mwenye uwezo wa kufanya kazi zinazohitaji utekelezaji wa haraka kwa usimamizi mdogo.
vii. Awe na uwezo wa kutunza siri na nyaraka za serikali katika nyanja zote.
viii. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta – Microsoft Office kama Word, Excel, PowerPoint.
Masharti ya jumla
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watu wa kuaminika.
iii. Maombi yote yataambatana na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne, au sita kwa wale walifika kiwango hicho.
iv. Uwasilishaji wa taarifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
v. Barua za maombi ziwasilishwe kwa Mkono kuletwa Masijala kwa njia ya Posta au Mkono.
vi. Watakaofanikiwa kuchaguliwa kwa ajili ya usaili watajulishwa kwa simu.
Soma zaidi: Jinsi ya Kujiunga TAESA Kupata Internship haraka